Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Esther Edwin Maleko
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza:- Je, upi mkakati wa kupata hatimiliki maeneo yanayomilikiwa na vituo vya wazee, watoto na taasisi za ustawi na maendeleo ya jamii?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ni upi mkakati maalum wa Wizara wa kuhakikisha maeneo ambayo bado hayajapata hati miliki yanaweza kupimwa na kupatiwa hati miliki ili kupunguza uvamizi kwenye maeneo hayo?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa maeneo mengi bado hayajaendelezwa, je, ni upi sasa mpango jumuishi wa Wizara kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanatumika vyema kwa ajili ya jumuiya zinazozunguka maeneo hayo?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Malleko, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi, Serikali imetenga shilingi milioni 75.7 kwa ajili ya ukamilishaji wa hatimiliki hizo ndani ya mwaka huu wa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la pili, Serikali ina mpango jumuishi wa kuhakikisha maeneo yote ambayo yanazunguka jamii kuna vituo vya afya, vituo vya kulelea watoto, mashamba darasa na viwanja vya kuchezea michezo ili kudhibiti viwanja hivyo visivamiwe. Ahsante.
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza:- Je, upi mkakati wa kupata hatimiliki maeneo yanayomilikiwa na vituo vya wazee, watoto na taasisi za ustawi na maendeleo ya jamii?
Supplementary Question 2
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa changamoto ya ukosefu wa hati miliki na uzio katika maeneo haya ya wazee imekumba Makazi ya Wazee Nunge, Vijibweni, Kigamboni, hali ambayo imeleta mgogoro mkubwa baina ya wananchi wa maeneo yale. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kufuatana na mimi kwenda kuona changamoto iliyopo katika Makazi ya Wazee ya Nunge, Kigamboni? (Makofi)
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMIII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kisangi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nipo tayari kufuatana na Mheshimiwa Mbunge nitakapomaliza Bunge hili kuona utaratibu mzuri wa Nunge ili tuweze kuukamilisha vizuri kwa kutenga fedha kwa ajili ya wananchi wetu. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved