Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 7 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 124 | 2024-09-04 |
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Uyui uliopangwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 utaanza?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania, imeendelea kuimarisha majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na kukarabati yaliyopo. Kutokana na uhaba wa majengo ya Mahakama, majengo haya yanajengwa na kukarabatiwa kwa awamu kwa kuzingatia mpango wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama na kadri ya fedha zinavyopatikana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia Mpango huo, jengo la Mahakama ya Wilaya ya Uyui linajengwa kwa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025. Kwa sasa taratibu za ununuzi wa kumpata mkandarasi zinaendelea. Nashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved