Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Uyui uliopangwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 utaanza?
Supplementary Question 1
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ni sababu gani zilifanya mradi huu usitekelezwe katika Mwaka wa Fedha wa 2023/2024?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, Serikali sasa ipo tayari kuongeza mradi wa kujenga nyumba za watumishi wa Mahakama katika mradi huu? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mradi huu awali ulipangwa kutekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, lakini kutokana na kwamba fedha za mradi huu zinapatikana kutoka kwa wadau wetu wa maendeleo hususani Benki ya Dunia, utekelezaji wa vigezo kwa ajili ya kupata fedha hii ulichelewa kukamilishwa na hivyo kusababisha fedha hizi kuvuka mwaka. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, sasa hivi fedha zimeshapatikana na ndiyo maana tupo kwenye hatua ya manunuzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, juu ya kujenga nyumba katika mradi huu, naomba nimwombe Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu mradi umeshapangwa ni kwa ajili ya kujenga Mahakama, kutakuwa na awamu nyingine ya kushughulikia nyumba za watumishi wa Sekta ya Mahakama. Kwa hivyo, awe na subira katika awamu itakayofuata tumeweka pia uboreshaji wa nyumba zikiwemo watumishi wa Mahakama upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui. Nashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved