Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 25 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 332 | 2024-05-14 |
Name
Mohammed Said Issa
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Konde
Primary Question
MHE. MOHAMED SAID ISSA aliuliza:-
Je, lini Serikali itakuwa na Hospitali Kuu ya Taifa moja ambayo itatoa huduma zote za afya bila kutegemea hospitali nyingine?
Name
Ummy Ally Mwalimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tanga Mjini
Answer
WAZIRI WA AFYA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Said Issa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, tayari Serikali ina Hospitali ya Taifa ambayo ni Hospitali ya Taifa Muhimbili. Aidha, kwa sasa hatua za kuiboresha hospitali hii zinatekelezwa ili kuweza kutoa huduma zote za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved