Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2015-2020 | Session 11 | Sitting 41 | Industries and Trade | Wizara ya Viwanda na Biashara | 541 | 2024-06-05 |
Name
Ameir Abdalla Ameir
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR aliuliza: -
Je, kwa kiasi gani ushirikiano kati ya TBS na ZBS unaleta matokeo chanya na kusaidia kutatua changamoto za wajasiriamali hususani kutoka Zanzibar?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekuwa na mashirikiano na Taasisi ya Viwango ya Zanzibar kwa maana ya (ZBS) kupitia Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding - MoU) ya zaidi ya miaka tisa sasa. Ushirikiano huu kati ya TBS na ZBS unaendelea kuleta matokeo chanya kwa kutatua changamoto za wajasiriamali wakiwemo kutoka Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuanzisha na kutekeleza mifumo ya uandishi wa viwango, usimamizi wa ubora, upimaji na ugezi na hivyo kusaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved