Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 13 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 165 2024-04-24

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Mkongo Gulioni pamoja na ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na la Upasuaji?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Mkongo ni moja ya vituo vya afya 202 vilivyofanyiwa tathmini kwa ajili ya ukarabati mkubwa ili viendane na mahitaji ya sasa ya utoaji wa huduma za afya.

Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kutafuta na kutenga bajeti kwa awamu ili kuwezesha uboreshaji wa miundombinu kwenye Kituo cha Afya Mkongo Gulioni, ahsante.