Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mariam Madalu Nyoka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Mkongo Gulioni pamoja na ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na la Upasuaji?
Supplementary Question 1
MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nataka pia, niende kwenye kituo kingine cha afya kilichopo Manispaa ya Songea. Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Mji Mwema ikiwa ni pamoja na wodi ya akina mama, wanaume, pamoja na OPD, kwani majengo yake ni chakavu?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Mariam Nyoka kwa namna ambavyo anaendelea kuwasemea wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na Watanzania kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, namhakikishia Mheshimiwa Mariam kwamba, tunafahamu Kituo cha Afya cha Mji Mwema katika Manispaa ya Songea ni moja ya vituo vikongwe na chakavu, lakini pia kina upungufu wa majengo ya huduma. Namhakikishia kwamba, tayari tumekiingiza kwenye orodha ya vituo 202 vya kuvikarabati kwa awamu ili viweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi, ahsante.
Name
Salma Rashid Kikwete
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mchinga
Primary Question
MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Mkongo Gulioni pamoja na ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na la Upasuaji?
Supplementary Question 2
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Je, Serikali inatuambia nini kuhusu Kituo cha Afya cha Rutamba kwa sababu, nimekiulizia mara kadhaa? Kituo kile hakijapangwa kwenye eneo lolote na ukizingatia kule idadi ya watu ni kubwa sana, tarafa ile haina kituo cha afya na kituo kile ni kichakavu sana, ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Mama Salma Kikwete kwamba, Kituo cha Afya cha Rutamba ni kituo kikongwe, lakini kinahudumia wananchi wengi, hakina miundombinu ya kutosha na tayari ameshalifuatilia sana.
Mheshimiwa Spika, namhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ina dhamira na inatafuta fedha. Wakati wowote fedha ikipatikana tutakwenda kukikarabati na kukipanua Kituo cha Afya cha Rutamba, ahsante.
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Mkongo Gulioni pamoja na ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na la Upasuaji?
Supplementary Question 3
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, mwaka 2023 Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa walitupatia fomu za kujaza kuchagua vituo vya afya vya kimkakati na tukaenda majimboni tukatoa taarifa kwa wananchi wote kwamba tutapewa fedha. Je, ni lini fedha hii itaingia ili kuendana na zile taarifa ambazo tumepeleka majimboni?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma za afya karibu zaidi na makazi yao.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tulileta fomu hapa Bungeni, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge, tulishaainisha kata za kimkakati kwa ajili ya kwenda kujenga vituo vya afya. Nawahakikishia kwamba Serikali bado ina mpango huo na tunaendelea kutafuta fedha. Mara fedha ikipatikana, maeneo yote ambayo yaliainishwa yatakwenda kujengewa vituo vya afya. Kwa hiyo, ahadi hiyo bado inafanya kazi, ni suala la muda tu, tutatekeleza, ahsante.
Name
Selemani Jumanne Zedi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukene
Primary Question
MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Mkongo Gulioni pamoja na ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na la Upasuaji?
Supplementary Question 4
MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Bukene ambacho kinahudumia Tarafa nzima ya Bukene yenye kata nane ni kikongwe, kimechakaa na kina upungufu wa majengo. Ni lini Serikali itatoa kipaumbele ili nacho kiweze kukarabatiwa, kiwe sawa na vituo vipya vinavyojengwa sasa hivi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Zedi kwa sababu ameleta orodha ya vituo vyake chakavu, kikiwemo Kituo cha Afya cha Bukene. Pia, nampongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nzega, ameleta orodha hiyo na pia, ameleta tathmini ya gharama inayohitajika kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa kituo hicho. Kwa hiyo, ni suala tu la muda tutatafuta fedha kwa ajili ya kwenda kutekeleza mpango huo, ahsante.
Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Mkongo Gulioni pamoja na ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto na la Upasuaji?
Supplementary Question 5
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi. Kituo cha Afya cha Changuge kimechoka na kimechakaa na Mheshimiwa Waziri alipita akakiona na akaahidi kukifanyia maboresho. Ni lini sasa kitatengewa fedha kwa ajili ya kufanyiwa maboresho?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Chagunge kipo kwenye orodha ya vituo 202. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba kitakarabatiwa, ahsante.