Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 13 Foreign Affairs and International Cooperation Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 177 2024-04-24

Name

Ameir Abdalla Ameir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR aliuliza: -

Je, upi mchango wa Lugha ya Kiswahili kwenye kukuza Diplomasia ya Uchumi?

Name

Amber. Mbarouk Nassor Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE (MHE. BALOZI MBAROUK NASSOR MBAROUK) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, lugha ya Kiswahili kwa sasa ni lugha rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Afrika. Aidha, kwa sasa kila tarehe 7 ya mwezi Julai ya kila mwaka inaadhimishwa kama siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani.

Mheshimiwa Spika, kwa muktadha huo, Lugha ya Kiswahili ni nyenzo muhimu katika kuwezesha mawasiliano duniani hususani katika shughuli za kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kitafiti na kisayansi. Hali hii inachangia moja kwa moja katika Diplomasia ya Uchumi kupitia ajira za wataalamu wa ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili, lakini pia huduma za ukalimani na tafsiri katika mataifa na mikutano mbalimbali na pia kutumika kama vyenzo wezeshi katika biashara.

Mheshimiwa Spika, aidha, lugha ya Kiswahili imekuwa ikitumika katika maelezo ya bidhaa mbalimbali na ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa, machapisho ya vitabu na tafiti mbalimbali za kisayansi ambayo yamekuwa yakiuzwa na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na kuchangia pato la Taifa, ahsante sana.