Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 9 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 146 | 2024-11-08 |
Name
Jacquline Andrew Kainja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaona umuhimu wa kuwezesha mawasiliano ya redio kwa Tarafa ya Kiwele, Kata za Kitunda, Uloli, Kilumbi na Kipili – Sikonge?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Utangazaji Tanzania limejenga mitambo ya kurushia matangazo ya redio masafa ya FM katika eneo la Usungilunde Kata ya Sikonge, Wilayani Sikonge ambapo TBC Taifa inapatikana katika masafa ya 87.9 MHz na Bongo FM masafa ya 89.9 MHz. Mitambo hii inafikisha matangazo umbali wa kilometa 60 za hewani (Air distance) kutoka Usungilunde. Kata ya Kitunda ipo umbali wa zaidi ya kilometa 130 za hewani, Uloli, Kilumbi na Kipili zipo umbali wa zaidi ya kilometa 140 za hewani, hivyo kutokufikiwa na matangazo ya TBC kutokea mnara uliopo Eneo la Usungilunde Kata ya Sikonge. Serikali kupitia TBC imeweka maeneo haya katika utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved