Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jacquline Andrew Kainja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza:- Je, lini Serikali itaona umuhimu wa kuwezesha mawasiliano ya redio kwa Tarafa ya Kiwele, Kata za Kitunda, Uloli, Kilumbi na Kipili – Sikonge?
Supplementary Question 1
MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante nami kupata nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na ukubwa wa Wilaya ya Sikonge na Tarafa ya Kiwele kutoka Kata ya Kitunda kwenda Kipili ni umbali wa kilometa za hewani 140. Je, Serikali kutokana na Mpango wa 2025 imepanga kuweka minara mingapi?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Jacqueline kwa ufuatiliaji wa mawasiliano ya uhakika kwa wananchi wa eneo hili lakini pili kama mwenyewe ulivyokiri ni umbali wa kilometa 140 wataalamu wetu wataendelea kufanya study ya kuona ni kiasi gani tuweze kuweka minara lengo ni kuhakikisha taarifa, mawasiliano, redio ziweze kusikika katika maeneo haya ambayo umeuliza.
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza:- Je, lini Serikali itaona umuhimu wa kuwezesha mawasiliano ya redio kwa Tarafa ya Kiwele, Kata za Kitunda, Uloli, Kilumbi na Kipili – Sikonge?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, usikivu wa Redio Tanzania katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Jimbo la Muhambwe ni hafifu sana, kama kule Kuninama, Mukabuye na Mkarazi hali inayochangia wananchi hawa kusikiliza redio za nchi jirani hivyo kukosa taarifa muhimu za nchi yao. Je, ni lini Serikali itaboresha usikivu wa Redio Tanzania katika vijiji vya pembezoni vya Jimbo la Muhambwe?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Florence, Mbunge wa Muhambwe, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosema maeneo haya ya pembezoni Redio Tanzania inasikika kwa mbali lakini tayari tupo kwenye mikakati TBC FM itaendelea kuchakata na kuona maeneo ya pembezoni pamoja na Muhambwe katika kijiji hiki ulichokisema tunaweza kuyafikia na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za ndani ya nchi kwa sababu Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kazi nyingi ni vyema wananchi wakapata taarifa kwa muda sahihi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved