Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 21 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 278 | 2024-05-08 |
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:-
Je, Serikali imefikia hatua gani katika kuwapatia vijana 400 vifaa vya kutengeneza vihenge visivyoruhusu hewa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC) imewapatia vijana 420 vifaa vya kutengeneza Vihenge vya Chuma visivyopitisha hewa vyenye thamani ya shilingi 548,479,105 ambapo kila kijana alipatiwa seti moja iliyojumuisha Arc Welding Machine, Angle Grinder Machine, Portal Grilling Machine, Steel Divider, Tape Measure, Try-square, Centre Push, Hand Hacksaw na Safety Goggles.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Vifaa hivi vilizinduliwa na kugawanywa kwa vijana 420 na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane tarehe 08/08/2023 katika viwanja vya maonesho vya John Mwakangale, Mbeya. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved