Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:- Je, Serikali imefikia hatua gani katika kuwapatia vijana 400 vifaa vya kutengeneza vihenge visivyoruhusu hewa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025?
Supplementary Question 1
MHE. NG’WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Kwanza nianze kwa kuishukuru na kuipongeza sana Serikali kwa majibu mazuri. Pia, nitumie fursa hii kuipongeza sana Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na hii ndiyo maana nzima ya kuahidi na kutenda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 - 2025 ukurasa wa 43 iliahidi kutoa vifaa hivi na kuwawezesha vijana 400, lakini jibu la Mheshimiwa Waziri linaonesha kwamba wamewawezesha vijana 420. Maana yake ni zaidi ya utekelezaji wa 100%. Sina swali la nyongeza, naipongeza Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwamba, naomba sasa kuwepo na series ya ufuatiliaji wa vijana hawa ili vifaa hivi walivyopewa viweze kweli kuwaletea yale manufaa ambayo yalitegemewa tangu mwanzo na manufaa kwa wakulima katika utunzaji wa chakula baada ya mavuno. Nashukuru sana. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: ahsante sana.
Name
Ussi Salum Pondeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chumbuni
Primary Question
MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:- Je, Serikali imefikia hatua gani katika kuwapatia vijana 400 vifaa vya kutengeneza vihenge visivyoruhusu hewa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025?
Supplementary Question 2
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha kiuchumi vijana ambao wapo katika Jimbo la Kibiti, ambapo ukipita Jimbo la Kibiti, ukiangalia mazingira watu wengi wanaonekana hali zao ni za chini. Sasa tunataka kujua Serikali yetu hii sikivu inawainuaje kiuchumi na ina mpango gani wa kuwawezesha...
MWENYEKITI: Sawa, umeeleweka. Mheshimiwa Waziri, majibu.
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, umenifahamu?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimweleze tu Mheshimiwa Mbunge kwamba suala lake lina wigo mpana, lakini katika Sekta ya Kilimo, moja ya malengo ya Serikali tuliyonayo kwa Jimbo la Kibiti hususan lile Bonde zima; ni kwamba sasa hivi tumeshatangaza tender kwa ajili ya kwenda kujenga mabwawa mawili makubwa kule na mifumo ya umwagiliaji. Kwa hiyo tukishatengeneza ile miundombinu kwenye maeneo yale maana yake vijana wengi wa Jimbo la Kibiti watanufaika na ile miradi. Kwa hiyo, watakuwa na shughuli za kiuchumi za kufanya. Hiyo ni kwenye Sekta ya Kilimo. Kwa sekta nyingine Waheshimiwa Mawaziri wengine wamesikia na watalifanyia kazi jambo hilo. Ahsante. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:- Je, Serikali imefikia hatua gani katika kuwapatia vijana 400 vifaa vya kutengeneza vihenge visivyoruhusu hewa kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025?
Supplementary Question 3
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa kuwa, Serikali imeanzisha Mpango wa Jenga Kesho Iliyo Bora kwa vijana nchini; je, ni lini Serikali sasa italeta Mpango huu katika ngazi za majimbo na halmashauri nchini? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mpango wa Jenga Kesho Iliyo Bora unaanza katika mwaka wa fedha unaokuja. Ndiyo maana katika bajeti ambayo Bunge lilitupitishia tumeainisha halmashauri 100 zitakazotenga maeneo kwa ajili ya vijana hao. Sisi Wizara tutakuja kwa ajili ya kujenga miundombinu yote. Shughuli hiyo ya kuwateua hao vijana itafanyika katika ngazi za majimbo na halmashauri husika. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved