Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 21 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 281 2024-05-08

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza:-

Je, nini mkakati wa Serikali katika kupunguza baadhi ya tozo na kufuta zingine ili kuleta unafuu kwa wavuvi?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2020 na mwaka 2022 Serikali ilifanya maboresho ya tozo mbalimbali ambapo ilipelekea baadhi ya leseni kuunganishwa na tozo nyingine kupunguzwa. Tozo ambazo zilipunguzwa ni ushuru wa zao la dagaa wanaozalishwa Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa na Bahari ya Hindi kutoka dola 0.16 hadi kufikia dola 0.1 kwa kilo na tozo ya dagaa wa Ziwa Tanganyika kutoka dola 0.5 hadi kufikia dola 0.3 kwa kilo. Pia, gharama za tozo ya kusafirisha minofu ya samaki ya sangara nje ya nchi ilipunguzwa kutoka dola 0.2 hadi kufikia dola 0.1 kwa kilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia, imepunguza ushuru wa uingizaji mazao ya bahari nchini kutoka dola 2.5 hadi kufikia dola 0.5 kwa kilo kwa mazao ya ngisi, pweza na kaa. Aidha, maeneo mengine ambayo yamefanyiwa maboresho ni kupunguza gharama ya ada za leseni za kusafirisha dagaa kutoka dola 1,000 hadi kufikia dola 250 kwa dagaa wa maji chumvi na maji baridi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara itaendelea kuboresha na kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi nchini kadiri itakavyowezekana na kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi katika Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.