Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 21 Finance Wizara ya Fedha 284 2024-05-08

Name

Cosato David Chumi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafinga Mjini

Primary Question

MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kurejesha 20% (Retention) ya Kodi ya Ardhi kwenye Halmashauri kama ilivyopitishwa katika Sheria ya Fedha 2023/2024?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwaka wa Fedha 2023/2024, Serikali ilifanya maboresho ya ukusanyaji wa kodi ya ardhi ambapo halmashauri kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI zinatakiwa kukusanya kodi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Hadi Aprili 2024, taratibu za kuwezesha halmashauri kuanza kukusanya kodi ya ardhi hazijakamilika, hususan kufungamanisha Mfumo wa Utunzaji wa Kumbukumbu za Ardhi na Mfumo wa Kukusanya Mapato ya Halmashauri (TAUSI). Hivyo, 20% inayopaswa kurejeshwa halmashauri itaanza mara tu zoezi la kukusanya kodi ya ardhi litakapoanza kutekelezwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, utaratibu huo unatarajiwa kuanza kabla au ifikapo 30 Juni, 2024.