Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cosato David Chumi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafinga Mjini

Primary Question

MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kurejesha 20% (Retention) ya Kodi ya Ardhi kwenye Halmashauri kama ilivyopitishwa katika Sheria ya Fedha 2023/2024?

Supplementary Question 1

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, sababu ya kuleta sheria hii ambayo tulipitisha hapa Bungeni ilikuwa ni kuzi-stimulate halmashauri kwa maana zitakapobakiwa na ile 20% itazisaidia, siyo tu katika kuboresha namna ya kukusanya, lakini pia kukusanya katika Sekta ya Ardhi kwa ujumla wake. Je, sisi kwa mfano mpaka sasa tumeshakusanya milioni 367, Serikali iko tayari kuturejeshea milioni 73.4 mara utaratibu utakapokuwa umeiva?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; tulikadiriwa tukusanye milioni 900 kwa maana kwamba 20% itakuwa milioni 180. Je, tutakapokuwa tumekamilisha wataturejeshea hizo fedha?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye maelezo yangu ya msingi ni kwamba utaratibu huu ambao unahusisha kurejesha utaenda sambamba na ukusanyaji kuanza kufanya kazi kwa kutumia TAMISEMI pamoja na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Kwa hiyo, mara utaratibu huu wa kufungamanisha mifumo utakapokuwa umekamilika na ukusanyaji kuanza mara moja na urejeshwaji nao utaanza kufanya kazi.