Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 37 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 483 2024-05-30

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kutafuta soko la uhakika la zao la mihogo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali imeendelea kuimarisha soko la Zao la Muhogo ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Masoko ya Muhogo na kuandaa majukwaa ya biashara yanayohusu zao hilo ili kutafuta soko la uhakika.

Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji huo, Wizara inaendelea na maandalizi ya ujenzi wa Soko la Muhogo la Kahama (Musoka) na miundombinu ya kukaushia muhogo katika Mkoa wa Kigoma ili kuendeleza biashara ya zao hilo.

Mheshimiwa Spika, Wizara imehamasisha wadau waliopo katika mnyororo wa thamani wa zao la Muhogo kujiunga pamoja na kuanzisha Chama cha Wazalishaji na Wasindikaji wa Zao la Muhogo Tanzania (TACAPPA). Uhamasishaji huo umewezesha kuuza nje ya nchi tani 21,620 za muhogo mkavu wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 7.6 kwa mwaka 2023. (Makofi)