Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 17 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 126 2024-11-07

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:-

Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa stendi kuu ya mabasi Babati ambayo ni Stendi Kuu ya Mkoa wa Manyara?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi katika Halmashauri ya Mji wa Babati unafanyika chini ya Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Miji ya Tanzania kwa Kuhusisha Ushindani “Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness’’ (TACTIC) awamu ya Pili. Utekelezaji wa mradi huo unaendelea ambapo kazi ya usanifu imekamilika na sasa maandalizi ya zabuni yanafanyika kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Umma wa NeST kwa ajili ya kumpata Mkandarasi na Mshauri Msimamizi kwa lengo la kuanza kazi za ujenzi. Ujenzi unatarajiwa kuanza Februari, 2025 baada ya kukamilika kwa taratibu za kumpata Mkandarasi.