Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa stendi kuu ya mabasi Babati ambayo ni Stendi Kuu ya Mkoa wa Manyara?

Supplementary Question 1

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali kutupatia fedha hizi zaidi ya bilioni 17 kwa ajili ya ujenzi huu naamini utakamilika. Nina swali moja tu, Mji wa Babati ni Makao Makuu ya Mkoa tuna uhitaji mkubwa wa ujenzi wa soko kuu. Je, Serikali iko tayari kututengea fedha kwa ajili ya soko kuu? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Halmashauri ya Mji wa Babati ni mji ambao unakua haraka, lakini una uhitaji mkubwa wa soko. Mheshimiwa Mbunge Gekul amefuatilia mara nyingi sana Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuona namna ambavyo wananchi wa Babati Mjini wanapata Soko Kuu. Ninaomba nimhakikishie tu kwamba tulishatoa maelekezo kwa Wakurugenzi wetu wa Miji na Halmashauri kuweka vipaumbele katika ujenzi wa masoko, lakini pia kuandika maandiko maalum kwa ajili ya maombi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa masoko hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI nimwelekeze Mkurugenzi wa Hamalshauri ya Mji wa Babati waandike andiko la mahitaji ya soko hilo na kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa ajili ya kuingizwa kwenye miradi ya kimkakati ili itafutiwe fedha kwa ajili ya ujenzi. Ahsante. (Makofi)

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa stendi kuu ya mabasi Babati ambayo ni Stendi Kuu ya Mkoa wa Manyara?

Supplementary Question 2

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na wingi wa watu katika Jimbo la Mbagala, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Stendi ya Mabasi ya Kusini pamoja na mabasi ya kwenda katikati ya Jiji la Dar es Salaam?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo yana sifa na yanahitajika kujenga stendi kwa ajili ya kusogeza huduma za jamii karibu zaidi na wananchi, kuongeza mapato ya halmashauri kwa kujenga stendi hizo. Ni kweli kwamba Jimbo la Mbagala ni moja ya majimbo yenye idadi kubwa ya wananchi na uhitaji wa stendi ni mkubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilishaanza kufanya utaratibu wa kutafuta eneo, lakini pia kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga stendi ya mabasi ya Kusini, lakini pia mabasi yanayokwenda katikati ya mji. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba suala hilo tutalifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nisisitize pia kwa Mkurugenzi kuweka kipaumbele kwenye bajeti za mapato ya ndani ya Manispaa ya Temeke ili kushirikiana na Serikali Kuu tuone namna nzuri ya kujenga stendi hiyo kwa ajili ya kuhudumia wananchi.

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa stendi kuu ya mabasi Babati ambayo ni Stendi Kuu ya Mkoa wa Manyara?

Supplementary Question 3

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Chemba unakua kwa kasi sana. Ninataka kujua ni lini sasa Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi, ambapo tayari andiko tumeshaleta kwenye Ofisi ya TAMISEMI. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Chemba walishawasilisha andiko la ujenzi wa stendi na tayari limeshafanyiwa uchambuzi katika ngazi ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI, na limeshawasilishwa Hazina. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Chemba kwamba Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hilo la stendi ya Chemba. Ahsante.

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa stendi kuu ya mabasi Babati ambayo ni Stendi Kuu ya Mkoa wa Manyara?

Supplementary Question 4

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya mkoa katika Mji wa Vwawa? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Hasunga na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Songwe mara nyingi wameulizia kuhusiana na ujenzi wa stendi ya Mkoa wa Songwe na Serikali siku zote tumewahakikishia kwamba, ni kipaumbele cha Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe tu, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mipango ya Serikali bado inaendelea na tunahakikisha kwamba tutapata fedha kwa ajili ya ujenzi wa Stendi ya Mkoa wa Songwe. (Makofi)