Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 427 2024-05-24

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza:-

Je, kuna mkakati gani wa Serikali kuongeza wigo wa barabara za lami katika Wilaya ya Kigamboni?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka 2023/2024 Serikali, kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ilitenga shilingi bilioni 2.88 ambazo zilitumika kujenga Barabara ya Tungi – Mjimwema na Chagani Polisi kilomita 2.3 na mifereji yenye urefu wa mita 3,800. Mwaka 2024/2025 zimetengwa shilingi bilioni 2.215 ambazo zitatumika kujenga Barabara ya Rombo Bar – RC Church, Kivukoni, Kivukoni P/S na umaliziaji wa Barabara ya Chagani – Polisi kwa kiwango cha lami kilomita 1.52 na mifereji yenye urefu wa mita 3,040.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia mkopo kutoka Benki ya Dunia inatekeleza Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II). Mradi huo utahusisha ujenzi wa kilomita 42.1 wa barabara za lami, mifereji ya maji ya mvua na madaraja. Hadi sasa mradi huo upo katika hatua za usanifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa barabara za lami katika miji, hivyo itaendelea kujenga barabara hizo zikiwemo za Manispaa ya Kigamboni kulingana na upatikanaji wa fedha.