Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 436 2024-05-24

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:-

Je, kwa nini Kada zinazowezesha utendaji kazi katika Hospitali hazijumuishwi pindi ajira zinapotangazwa?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa utaratibu wa ajira wa kada ambazo ni saidizi mfano Wahasibu, Maafisa Ugavi na Madereva unafanywa na Sekretarieti ya Ajira na Utumishi na hivyo hazijumuishwi katika kada za Watumishi wa Afya mfano Madaktari, Wauguzi, Wafamasia na Maabara ambao utaratibu wa ajira husimamiwa na Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kupunguza tatizo hili tutaboresha mikakati ya mawasiliano ndani ya Serikali kwa kuonesha mahitaji halisi ya kada hizi ili vibali vya ajira vinavyotolewa vizingatie pia mahitaji ya kada hizo kwa Wizara ya Afya, ahsante.