Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Conchesta Leonce Rwamlaza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Je, kwa nini Kada zinazowezesha utendaji kazi katika Hospitali hazijumuishwi pindi ajira zinapotangazwa?
Supplementary Question 1
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwamba Serikali imetambua kuwepo kwa kada hizi ambazo zinawezesha hospitali zetu kufanya kazi. Pamoja na kutaja wale uliowataja lakini kuna watu wa TEHAMA, watu wa mifumo ya maji, mifumo ya umeme, ma-engineer wa ujenzi na Maafisa Habari.
Je, ni kwa nini Wizara ya Afya isiweze yenyewe kuajiri watu hawa na kuwapa ajira za kudumu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera hawa wote niliowataja wameajiriwa na hospitali na inawezekana hata katika sehemu nyingine. Hospitali kutokana na mapato yao wanaelemewa mzigo, wanashindwa kuwalipa mishahara mizuri na kwa wakati unaotakiwa…
MWENYEKITI: Swali Mheshimiwa Mbunge.
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Je, Serikali haioni sasa iwapunguzie kabisa mzigo hospitali ili iweze kuwalipa hawa wawezeshaji na wenyewe wafaidi mishahara? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu kwa namna ambavyo ameuliza maswali yake, inaonekana ni kwa namna gani anafuatilia vizuri eneo hili letu la afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge na nimtoe wasiwasi, kwanza ajira ya kudumu haitokani na kuajiriwa na Wizara ya Afya. Ajira ya kudumu haipatikani kwa sababu wameajiriwa na Wizara ya Afya ila kwa kushirikiana na Utumishi, tumekuwa tukiwaajiri watu wote hawa. Kwa mfano, leo ndani ya Wizara ya Afya na hospitali zetu zote kuna watu wa IT, watu wa kada nyingine zote ambao wana ajira za kudumu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa juhudi za watumishi wetu na Wakurugenzi wa hospitali zetu, wamekuwa wenyewe wakizalisha mapato yao ya ndani na wakiweza kuajiri kuziba yale ma-gap ambayo Serikali haijaweza kuajiri watu hao, lakini Serikali imeweka utaratibu kila wakati vibali vya ajira vinapotoka wanahakikisha hao ambao tayari wanajitolea wanakuwa accommodated kwenye ajira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea kufanya mawasiliano na Serikali kama nilivyosema ili kwa kweli hawa wenzetu ambao tayari wamewaajiri wameshazoea mazingira na wanafanya kazi ndani ya hospitali zetu wawe kila wakati wanakuwa accommodated ndani ya vibali vinavyotoka kila wakati. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved