Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 33 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 437 | 2024-05-24 |
Name
Maimuna Ahmad Pathan
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MAIMUNA S. MTANDA K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza:-
Je, lini Mikoa ya Lindi na Mtwara itapata Mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Rufiji ambao upo jirani?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Ahmad Pathan, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kufikia malengo ya kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi kwa 95% mijini na 85% vijijini ifikapo 2025 kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maji kwa kutumia vyanzo vya maji vya uhakika ikiwemo maziwa, mito na mabwawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza azima hiyo, Serikali inaendelea na mapitio ya usanifu wa mradi wa kutoa maji katika Mto Ruvuma kwenda kwenye Mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na maeneo ya pembezoni yatakayopitiwa na bomba kuu. Aidha, Serikali inaendelea na tathmini ya awali ya usanifu wa mradi wa maji wa kutoka Mto Rufiji kupeleka kwenye Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa lengo la kuhakikisha inaongeza hali ya upatikanaji wa maji katika Mikoa hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zote hizo zinatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved