Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 33 Finance Wizara ya Fedha 438 2024-05-24

Name

Abdi Hija Mkasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Micheweni

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO K.n.y. MHE. ABDI HIJA MKASHA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kurejesha huduma za Kibenki za CRDB, NMB na PBZ katika Wilaya ya Micheweni?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kabla ya benki kufanya uamuzi wa kufungua tawi jipya, benki husika hufanya upembuzi yakinifu ukiwa na lengo la kuangalia kama kuna uwepo wa biashara ya kutosha ambayo italeta faida kwa benki husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki za CRDB, NMB na PBZ kwa sasa hazina matawi katika Wilaya ya Micheweni. Hata hivyo, Wananchi wa Wilaya ya Micheweni wanapata huduma za kibenki kutoka benki hizo kupitia jumla ya mawakala 27 (CRDB 11, NMB 12 na PBZ 4).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kadhalika Benki Kuu tayari imetoa idhini kwa Benki ya PBZ kufungua tawi katika eneo la Konde lililopo katika Wilaya ya Micheweni, na matayarisho ya kufungua tawi hilo yanaendelea, ahsante.