Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 440 2024-05-27

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Nandembo - Kitula hadi Nampungu - Tunduru kwa kiwango cha lami?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Nandembo - Nampungu ina urefu wa kilometa 28.81 ambapo katika mwaka 2021/2022, yalifanyika matengenezo ya tabaka la changarawe kilometa 27.3 na kilometa 1.51, tabaka la udongo kwa gharama ya shilingi milioni 241. Aidha, Serikali imepanga kufanya usanifu wa Barabara ya Nandembo – Nampungu kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kadri ya upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuhudumia barabara za Mji Tunduru kwa kuzijenga, kuzifanyia matengenezo na kuzikarabati kulingana na upatikana wa fedha.