Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Nandembo - Kitula hadi Nampungu - Tunduru kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; Barabara ya kutoka Kangomba – Ipanje - Kidodoma- Legezamwendo hadi Machemba lini itatengenezwa ili iweze kupitika muda wote? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Serikali ina mpango gani wa kutengeneza Barabara ya kutoka Pacha ya Mwongozo kupita Mchuruka hadi Cheleweni ili nayo iweze kupitika muda wote?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifanya kazi kubwa sana ya kufuatilia maendeleo ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Ruvuma.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la kwanza, Barabara ya Kangomba – Ipanje – Kidodoma - Legezamwendo hadi Machemba yenye urefu wa kilometa 85 tayari Serikali imekuwa ikitenga fedha katika kila mwaka wa fedha kuhakikisha barabara hiyo inapitika kwa misimu yote. Katika mwaka 2022/2023 shilingi milioni 250 zilitolewa kwa ajili ya kuchonga na kuweka kifusi kwenye barabara hiyo lakini mwaka 2023/2024 shilingi milioni 350 zimetengwa kwa ajili ya kuchonga na kuweka kifusi pia kuweka makalvati manne.

Mheshimiwa Spika, pia katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, shilingi milioni 270 zimetengwa kwa ajili ya kurekebisha maeneo korofi yaliyobaki ambayo yana urefu wa kilometa 20. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge baada ya marekebisho haya ya mwaka wa fedha 2024/2025, barabara hii itakuwa imekamilika na itakuwa inapitika mwaka mzima.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili kuhusu Barabara ya Mwongozo – Mchuruka - Cheleweni katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, shilingi milioni 61.32 zimetolewa kwa ajili ya kurekebisha sehemu korofi yenye urefu wa kilometa 9.41. Katika mwaka wa bajeti 2024/2025 shilingi milioni 18 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa makalvati matatu kwenye maeneo korofi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali itaendelea kutenga fedha kuhakikisha inaboresha na inakarabati miundombinu ya barabara katika majimbo yote ya Mkoa wa Ruvuma. (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Nandembo - Kitula hadi Nampungu - Tunduru kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali iliahidi kujenga kilometa mbili za lami kwa kila makao makuu ya halmashauri mpya na Mheshimiwa Bashungwa akiwa Waziri wa TAMISEMI aliwaahidi Wananchi wa Nyamwaga barabara ya kilometa mbili kwa kiwango cha lami...

SPIKA: Swali.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujua ni lini ahadi hiyo ya Mheshimiwa Waziri itatekelezwa katika Mji wa Nyamwaga? Ahsante

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha kwamba inaboresha miundombinu na hasa kwenye barabara zetu hizi za wilaya. Nimhakikishie Serikali itahakikisha inatafuta pesa kuhakikisha inajenga barabara aliyoitaja.
SPIKA: Mheshimiwa Boniphace Nyangidu Butondo, Mbunge wa Kishapu, sasa aulize swali lake.