Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 441 2024-05-27

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza:-

Je, lini fedha za kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mji wa Mhunze Wilayani Kishapu kwa kiwango cha lami zitatolewa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuzifanyia usanifu barabara zote kuu na muhimu za Mji wa Mhunze kutoka tabaka la udongo na changarawe kwenda tabaka la lami ambapo kilometa mbili za Barabara za DED - DC kilometa moja na Madukani kilometa moja zimejengwa kwa tabaka la lami kwa gharama ya shilingi bilioni 1.07. Aidha, katika mwaka 2024/2025, Serikali imetenga bajeti ya shilingi milioni 680 kwa ajili ya ujenzi wa tabaka la lami kilometa moja Barabara ya Madukani.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kila mwaka mpaka kukamilisha barabara muhimu za Mji wa Mhunze Wilayani Kishapu kwa kiwango cha lami.