Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza:- Je, lini fedha za kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mji wa Mhunze Wilayani Kishapu kwa kiwango cha lami zitatolewa?

Supplementary Question 1

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Naomba niulize maswali maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; mwaka 2015 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Magufuli aliahidi kilometa nne katika Mji wa Mhunze na mpaka sasa kilometa moja imetekelezwa katika ujenzi. Serikali inasema nini juu ya kilometa tatu zilizobaki kwa ajili ya kuzitekeleza?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; tumekuwa tukipokea fedha za mfuko wa jimbo, tozo na road fund katika usawa sahihi kwa pamoja kwa maana ya kwamba, zimekuwa zikitolewa katika kila halmashauri kwa usawa lakini kiukweli mitandao ya barabara inatofautiana wilaya hadi wilaya. Kwa nini Serikali isije na formula mpya ya kutoa mgao wa fedha kulingana na ukubwa wa mtandao wa barabara katika kila wilaya? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifanya kazi kubwa sana ya kuwatumikia wananchi wake.

Kuhusiana na swali la kwanza, naomba nimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kwamba kipaumbele cha Serikali ni kuhakikisha ahadi za Viongozi Wakuu zinatekelezwa. Kama alivyosema yeye mwenyewe tayari katika barabara hii ya Mji wa Mhunze ambayo iliahidiwa kilometa nne tayari kilometa moja imeshajengwa kwa lami. Nimhakikishie katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 shilingi milioni 688 zimetengwa kwa ajili ya kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami lakini na kuweka taa. Kwa hiyo, nikuhakikishie ahadi ile iliyotolewa na Hayati Magufuli ya kilometa nne inaendelea kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili; kusema kweli Mheshimiwa Mbunge hoja yako ni ya msingi na Serikali imelitambua hilo na tayari Serikali inafanya mchakato ili kutengeneza formula mpya ambayo itazingatia mambo kadha wa kadha ikiwemo urefu wa mtandao wa barabara katika jimbo husika katika mgao wa fedha hizi kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika kila jimbo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mbunge, hoja yake ni ya msingi Serikali inaendelea nayo na katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, utaratibu mpya wa kutoa fedha hizi utaanza kutumika.

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza:- Je, lini fedha za kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mji wa Mhunze Wilayani Kishapu kwa kiwango cha lami zitatolewa?

Supplementary Question 2

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Barabara ya Jimbo la Kilolo kutoka Mtandika hadi Nyanzwa kilometa 40 ni mbovu mno na ni muhimu kwa uchumi. Je, lini itajengwa hata kwa kiwango cha changarawe?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inakusudia kutafuta fedha na kuhakikisha kwamba barabara hiyo inajengwa ili iweze kuwa na manufaa kwa ajili ya wananchi.

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza:- Je, lini fedha za kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mji wa Mhunze Wilayani Kishapu kwa kiwango cha lami zitatolewa?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itajenga barabara za lami angalau hata kilometa mbili kwenye Mji mdogo wa Himo? Ahsante.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali inatafuta fedha na itahakikisha kwamba inakuja kujenga barabara hiyo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge.