Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 34 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 446 | 2024-05-27 |
Name
Taska Restituta Mbogo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto, Wodi ya watoto na wodi ya wanaume Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi utakamilika?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni tano kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la Mama na Mtoto, wodi ya watoto na wodi ya wanaume katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi lenye sehemu mbili ambazo ni Wing A na Wing B. Aidha eneo la Wing A limekamilika kwa 98% ambapo tayari linatumika kwa huduma za wagonjwa wa nje na huduma za Radiolojia na eneo la Wing B limefikia 20% na ujenzi unaendelea. Naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved