Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 447 2024-05-27

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia watoto kupata matibabu baada ya kufuta Toto Afya Kadi huku tukisubiri Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, mfumo wa kulipia bima za watoto kupitia Toto Afya Kadi umebadilika na kwa sasa unafanyika kupitia utaratibu wa shule na vifurushi vya bima ya afya vya najali, wekeza na timiza ambapo wanajiunga kupitia wazazi wao.

Mheshimiwa Spika, kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote utawezesha makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo watoto kupata huduma za afya kwa urahisi pasipo kuwa na vikwazo, naomba kuwasilisha.