Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 34 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 450 2024-05-27

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:-

Je, upi Mkakati wa Serikali kuhakikisha wajasiriamali wadogo wanakuwa sehemu ya wawekezaji wa ndani kupitia shughuli zao?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Elias Mahawanga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, uwekezaji ni dhana pana ambayo imegawanyika katika kundi la uwekezaji mdogo sana, mdogo, wa kati na mkubwa. Hivyo, wajasiriamali wadogo ni sehemu ya wawekezaji wa ndani wanaotoa mchango mkubwa katika uchumi kwa kutoa ajira na kukuza kipato cha mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali ni kuendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wajasiriamali wadogo ikiwemo mafunzo ya ujasiriamali, mikopo ya riba nafuu, kujenga miundombinu ikiwemo majengo/mitaa ya viwanda na biashara, kuwapatia nembo ya ubora na kuwatafutia masoko kupitia taasisi za CBE, SIDO, TBS na TANTRADE. Huduma zote hizi zinawasaidia wajasiriamali kukua na hatimaye kuwa wawekezaji wakubwa.