Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 49 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 629 2024-06-19

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza:-

Je, lini Bajeti ya Barabara za Wilaya ya Missenyi zenye Mtandao wa Kilometa 921 itaongezwa ili barabara hizo zitengenezwe kwa ubora?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kutoa taarifa kuwa, Serikali imeshaongeza bajeti ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara za Wilaya ya Missenyi kutoka shilingi milioni 723.85 mwaka 2020/2021 hadi shilingi bilioni 2.42 mwaka 2023/2024.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya kutengeneza barabara kwa nchi nzima kadri ya upatikanaji wa fedha ikiwemo kuongeza bajeti kwa Wilaya ya Missenyi.