Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 49 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 630 2024-07-19

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa Barabara ya Kibondo Mjini yenye urefu wa Kilometa sita kwa kiwango cha lami kama ilivyotolewa na Rais wa Awamu ya Tano?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa barabara za lami Kibondo Mjini ambazo zitachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi. Kati ya mwaka 2019/2020 hadi 2023/2024, jumla ya kilometa 5.85 za barabara za lami zimejengwa na kukamilika katika Mji wa Kibondo. Ujenzi wa kilomita 2.5 kwa tabaka la lami unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mpango wa bajeti wa mwaka 2024/2025, zitajengwa barabara za lami kilomita 1.37. Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) itaendelea kuihudumia na kuiboresha miundombinu ya barabara za Kibondo Mjini kadri fedha zinavyopatikana. (Makofi)