Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 49 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 633 2024-06-19

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya Uvinza pamoja na Mahakama za Mwanzo Kalya na Buhingu?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Wilaya ya Uvinza ni miongoni mwa Mahakama 18 za Wilaya zilizojengwa na Serikali katika Mwaka wa Fedha 2022/2023. Ujenzi wa Mahakama hii ulikamilika na kuanza kutoa huduma za kimahakama tangu mwaka 2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulingana na Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama, Mahakama ya Mwanzo ya Buhingu imepangwa kujengwa katika Mwaka wa Fedha 2024/2025. Aidha, kadri fedha zitakapopatikana Mahakama ya Mwanzo Kalya itajengwa.