Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nashon William Bidyanguze
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Kusini
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya Uvinza pamoja na Mahakama za Mwanzo Kalya na Buhingu?
Supplementary Question 1
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Kwanza naomba nikiri kwamba Mahakama ya Wilaya ya Uvinza imeshajengwa na hili swali ni la siku nyingi sana na limekuja tena mara ya pili. Niliacha kulizuia lisiulizwe kwa sababu ya hizi mahakama mbili; sasa ninafahamu kwamba mwaka wa fedha 2023/2024, Mahakama ya Buhingu ilitengewa fedha kwa ajili ya kujengwa, lakini ujenzi ule haukufanyika. Swali la kwanza; je, ni lini fedha hizi zitakuja kwa ajili ya kujenga hiyo Mahakama ya Mwanzo ya Buhingu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; zipo Mahakama ya Nguruka, Uvinza na Ilagala, Mahakama hizi zimechakaa sana, je, ni lini zitapelekewa fedha kwa ajili ya ukarabati? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiri kwamba ni kweli ilipangwa bajeti katika mwaka wa fedha uliopita, lakini hadi mwaka unamalizika fedha hiyo haikuweza kutoka. Hivi sasa nimpe uhakikisho Mheshimiwa Mbunge wa Kigoma Kusini, kwamba Mahakama hii ya Buhingu taratibu sasa hivi zilizofikiwa ni kwenye hatua ya manunuzi kwa maana ya fedha zipo, mara taratibu zitakapokamilika ujenzi wa Mahakama hii utaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Mahakama ya Uvinza na Ilagala ambazo ni za muda mrefu, tunakiri kuwepo kwa Mahakama ambazo zinahitaji ukarabati au kujengwa upya kulingana na kiwango cha uharibifu au uchakavu na kama nilivyosema kwenye jibu la msingi kadri hali ya fedha itakavyoruhusu Mahakama zote hizo zitakarabatiwa.
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya Uvinza pamoja na Mahakama za Mwanzo Kalya na Buhingu?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Shinyanga ina halmashauri mbili, Halmashauri ya Shinyanga ipo mbali na mjini na Mahakama ipo mjini pale manispaa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga Mahakama yenye hadhi ya wilaya katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wazo la Mheshimiwa Mbunge, linapokelewa lakini katika mpango wa Mahakama ambao ni sehemu ya Serikali Kuu ni Mhimili unaozingatia sehemu ya Serikali Kuu tunapenda kujenga Mahakama hizi Makao Makuu ya Wilaya ambapo kuna DC kama unavyofahamu usimamizi wa nidhamu na maadili ya Mahakimu wa ngazi ya wilaya husimamiwa na waheshimiwa ma-DC. Kwa hiyo, tunapendelea zaidi kwenye ngazi ya wilaya tuwe na Mahakama moja ya ngazi ya wilaya. Kwa hiyo, ninafahamu changamoto aliyonayo, lakini kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu hizi huduma zitapelekwa karibu na wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana ya kupunguza adha kule Shinyanga kuna Mahakama za mwanzo ambazo zinajengwa. Katika Mkoa wa Shinyanga tunajenga, Kishapu kama wilaya kutakuwa na Mahakama ya Wilaya mwaka huu, lakini zipo Mahakama nyingine mbili za mwanzo zinajengwa kama juhudi za Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kupeleka huduma za haki karibu zaidi na wananchi maeneo ya Malunga na maeneo ya Majengo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved