Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 49 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 640 2024-06-19

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:-

Je, Serikali imejipangaje katika kuhamasisha kilimo hai kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula, nguo na vipodozi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo hai ni mfumo ambao unazingatia usalama wa rasilimali za uzalishaji, hifadhi ya mazingira, afya ya walaji na kuongeza kipato. Hapa nchini, kilimo hai kinatumika katika uzalishaji wa mazao ikiwemo pamba, kahawa, kakao, chai na mazao ya bustani kulingana na mahitaji ya soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhamasisha kilimo hai kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya masoko mbalimbali Wizara inatekeleza yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeandaa na kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Kilimo Ekolojia Hai wa mwaka 2023 – 2030; kusimamia mikataba ya kilimo hai katika mazao ya pamba, kahawa, kakao, chai na mazao ya bustani; kutoa elimu ya kilimo hai na hifadhi ya mazingira kwa wakulima kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo mashamba darasa; na kufanya utafiti wa matumizi sahihi ya viuatilifu kwa lengo la kulinda ekolojia na kuwezesha kilimo endelevu.