Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje katika kuhamasisha kilimo hai kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula, nguo na vipodozi?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza sana hatua ya Serikali kwa kupitisha mkakati wa kilimo hai ekolojia wa mwaka 2023 mpaka 2030 hii ni component muhimu sana. Swali la kwanza; je, Serikali katika bajeti hii ya kilimo iliyosheheni fedha imetenga kiasi gani kwa ajili ya kuendeleza mkakati wa kilimo hai ekolojia ambao una mwelekeo wa kuwanufaisha wakulima wetu na kuwatajirisha? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, vipi lile dawati la kilimo hai kwenye Wizara bado lipo hai? Kwa isivyo bahati aliyekuwa anashughulika na dawati hili Mwenyezi Mungu alimpenda tangu hapo hatujasikia mwingine. Sasa kwa kuwa tunataka shughuli za kilimo hai ziendelee, tunataka uhakika huyu mtu ameshakuwa-replaced? Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tumetenga bajeti kwa ajili ya kusimamia kilimo hai na ukiangalia pale, tuna kifungu kabisa kime-state amount ambayo itatumika kwa ajili ya kusimamia zao hili ambayo siyo chini ya shilingi milioni 200 na katika moja ya mkakati mkubwa tulionao tumeiteua Bihawana kuwa moja ya centre of excellence kwa mazao haya ya kilimo hai ekolojia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu dawati, dawati lipo hai na tayari tumeshamteua msimamizi tarehe 6 Juni, 2024, tayari mtu ambaye anasimamia dawati la kilimo hai pale Wizarani amepatikana kupitia katika ule mkutano na nimthibitishie tumepata vilevile wawekezaji ambao wapo tayari kutu-support katika uendelezaji wa kilimo hai ekolojia. Ahsante.

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje katika kuhamasisha kilimo hai kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula, nguo na vipodozi?

Supplementary Question 2

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali la nyongeza kuhusu wakulima wale walioathirika na mafuriko, siyo Rufiji peke yake ambapo wakulima wa mpunga wameathirika na mafuriko. Swali langu, je, Serikali haioni haja ya kuwapatia mbegu na mbolea ya dharura wananchi wote (wakulima) wa maeneo yote yanayolima mpunga ambao wameathirika na mafuriko katika msimu ujao? Ninakushukuru.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana katika ile tathmini tumeainisha watu wote ambao wameathirika wale ambao wanahitaji msaada kutoka Serikalini. Kwa mfano, katika maeneo ya Kibiti pamoja na Rufiji tayari tumeshaainisha na tunaendelea kuainisha na maeneo mengine yakiwemo katika jimbo lako. Kwa hiyo tutakapomaliza hiyo tathmini yetu maana yake na wenyewe tutawafikia kwa sababu miongoni mwa misaada tunayotoa ni pamoja na mbolea na mbegu.

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje katika kuhamasisha kilimo hai kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula, nguo na vipodozi?

Supplementary Question 3

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa wakati Mheshimiwa Naibu Waziri anataja hukuitaja Rukwa kwamba na wao wamefikiwa. Kata zote za pembezoni mwa mwambao wa Ziwa Tanganyika wamepata hiyo athari ya mafuriko. Kwa kuwa hawakuwa kwenye chanzo cha maji isipokuwa ni mabadiliko ya tabianchi. Ni lini na wao watafikiwa wapewe msaada huo? Ninakushukuru.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilipokee swali la Mheshimiwa Mbunge ili tutume timu yetu ikafanye tathmini na kuona ukubwa wa tatizo na watu gani wanahitaji Serikali iweze kuwasaidia kwa sababu haya yapo katika mpango wetu na tunaweza kuyatekeleza. Ahsante.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje katika kuhamasisha kilimo hai kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula, nguo na vipodozi?

Supplementary Question 4

MHE. SAASISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kata ya Kia na Kata ya Muungano ambao wanahudumiwa na Mto Johari walipata mafuriko na tunashukuru Serikali ilituletea chakula, lakini chanzo cha mafuriko yale kinasababishwa na kukosekana na ukuta unaozuia maji kwenda kwenye mashamba ya wananchi. Je, Serikali ipo tayari na ni lini itaenda kujenga ukuta ili kuzuia maji yasipande kwenye mashamba ya wananchi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujenga lazima tufanye tathmini na sisi tutatuma timu yetu ya Tume ya Umwagiliaji ili waweze kufika katika hizo kata mbili ulizozitaja za Kia na Muungano na baada ya ile tathmini maana yake tutatafuta fedha ili tujenge tuweze kuwasaidia wananchi katika kipindi kinachofuata. (Makofi)