Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 1 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 1 | 2025-01-28 |
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:-
Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 na 2021/2022 Kituo cha Afya Kisiwani kilipokea jumla ya shilingi milioni 490 kwa ajili ya ujenzi wa majengo matano ambayo ni: Jengo la Maabara; Jengo la kufulia; Jengo la Upasuaji; Jengo la Wazazi; Kichomea taka; na nyumba ya mtumishi (three in one (3 in 1)). Majengo yote yamekamilika na yanatoa huduma ikiwemo huduma za dharura na upasuaji kwa mama mjamzito.
Mheshimiwa Spika, awamu ya pili ya ujenzi wa kituo hiki itahusisha ujenzi wa wodi ya wanawake, wanaume na watoto. Serikali itaendelea kutekeleza ujenzi huu kwa awamu na Kituo cha Afya cha Kisiwani kitapewa kipaumbele. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved