Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 1
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa kituo hiki kinahudumia kata tatu: Kata ya Mshewa, Msindo na Kisiwani hivyo kina wananchi wengi sana ambao wanahudumiwa katika kituo hiki; na wodi ya wanawake na wanaume hazipo kabisa hivyo, anapotokea mgonjwa ni lazima apelekwe katika Hospitali ya Wilaya ya Same, kilometa 30. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa majengo haya ili kusogeza huduma kwa wananchi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kituo hiki kiko karibu na makaburi, kwa sababu hiyo wagonjwa waliolazwa pale hususan wodi ya mama na mtoto wanaona matukio yote ambayo yanaendelea wakati wa mazishi, hivyo huwa na hofu sana. Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga uzio kwa haraka katika kituo hiki? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la kwanza, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana na uhitaji wa kituo hiki cha afya na ndiyo maana tayari Serikali ilishaleta shilingi milioni 490 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya awali. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea na awamu ya pili, ambapo Serikali italeta fedha kwa ajili ya kujenga wodi ya wanawake, wanaume pamoja na watoto. Serikali itafanya hivyo kwa kuzingatia umuhimu mkubwa sana wa huduma inayotolewa katika kituo hiki cha afya.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili ambalo linahusiana na suala zima la uzio. Ninaomba nichukue nafasi hii kumkumbusha Mkurugenzi wajibu wa msingi, aweze kufanya tathmini katika eneo la hiki kituo cha afya ili ajue gharama zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa fence na kupitia mpango na bajeti katika halmashauri inayotokana na mapato ya ndani, waweze kutenga fedha kwa ajili ya kuanza kujenga uzio huu na pale nguvu itakapopungua Serikali Kuu itakuja kuongezea lakini, Mkurugenzi aanze kazi hii. (Makofi)
Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 2
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi, ninaomba kuuliza swali la nyongeza, Tarafa ya Mgeta ina kata saba na ina kituo kimoja cha afya....
SPIKA: Swali.
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Spika, ninaomba kuuliza swali, je, ni lini Serikali itatuongezea Kituo kingine cha Afya katika Tarafa ya Mgeta?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri ya uwakilishi anayoifanya katika jimbo lake.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie kwamba, katika mwaka huu wa fedha Serikali italeta fedha za kuanzia, shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza kujenga vituo vya afya vya kimkakati katika kila jimbo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, ninaomba nikuhakikishie na wewe utakuwa miongoni mwa Wabunge watakaopokea fedha hizi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kwenye majimbo yao.
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 3
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapeleka fedha za kujenga Kituo cha Masieda – Gembakw, ambako tulishaweka kwenye mpango wa kujengewa? Ahsante.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama nilivyotangulia kusema, kwamba katika mwaka huu wa fedha Serikali italeta shilingi milioni 250 za kuanza ujenzi wa kituo cha afya cha kimkakati katika kila jimbo. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na yeye katika jimbo lake fedha hizi zitamfikia.
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 4
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali italeta fedha za kujenga kituo cha afya katika Tarafa ya Nambis, ambako ni miaka minne tumeomba?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Zacharia Issaay kwamba katika mwaka huu wa fedha shilingi milioni 250 zitapelekwa katika jimbo lake kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo cha afya cha kimkakati. (Makofi)
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapeleka pesa katika Kata ya Image? Kwa sababu wodi na maabara zinatakiwa ili wananchi wasiende umbali mrefu kufuata matibabu. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa kuendelea kuimarisha miundombinu katika vituo vyetu vya kutolea huduma ya afya msingi. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari fedha zimekuwa zikitoka kwa awamu kwa ajili ya kuboresha vituo vyetu hivi vya kutolea huduma za afya msingi. Nimhakikishie Serikali itaendelea kuleta fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu aliyoitaja.
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 6
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itapeleka pesa kwa ajili ya kumalizia jengo la OPD katika Kituo cha Afya cha Chiungutwa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mchungahela kwamba, Serikali tayari imekuwa ikileta fedha, kwa ajili ya kuanza kujenga majengo ya awali. Pia Serikali inajenga miundombinu hii katika vituo vyetu hivi vya afya na vituo vya kutolea afya msingi kwa awamu. Nimhakikishie, kwa awamu inayofuata Serikali itaweka kipaumbele kikubwa sana, kwa ajili ya kukamilisha majengo haya ya OPD katika kituo hiki cha afya.
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 7
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali italeta fedha kwenye Kituo cha Afya Nyang’hwale, kwa ajili ya kujenga jengo la X–Ray?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Hussein Amar kwamba, Serikali inaleta fedha kwa awamu, kwa ajili ya kuendeleza miundombinu katika vituo vyetu vya kutolea huduma ya afya msingi. Pia, kama alivyoainisha, Jengo hili la X–Ray, Serikali italeta fedha, kwa ajili ya kuhakikisha linajengwa, ili liweze kuanza kutoa huduma hizi kwa wananchi.
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 8
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wa kujenga majengo muhimu katika Kituo cha Afya cha Mile Tano, Jimbo la Tabora Mjini?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Hawa Mwaifunga kwamba, Serikali inajenga miundombinu katika vituo vyetu vya kutolea afya msingi kwa awamu. Tayari imejenga majengo ya awali na inaendelea kuleta fedha kwa awamu, kwa ajili ya kuboresha na kukamilisha miundombinu mingine katika vituo vyetu hivi vya kutolea huduma ya afya msingi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge fedha zitapelekwa kwa ajili ya kuendeleza kujenga miundombinu katika kituo hiki cha afya alichokitaja.
Name
Miraji Jumanne Mtaturu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mashariki
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 9
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali italeta fedha, kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la theatre katika Kituo cha Afya Ntuntu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mtaturu kwamba, Serikali inafahamu umuhimu mkubwa sana wa vituo vyetu vya kutolea huduma ya afya msingi na ndiyo maana inaleta fedha kwa awamu, kwa ajili ya kuvijenga na kuviendeleza vituo hivi. Kwenye hicho kituo cha afya alichokitaja na jengo hili la theatre, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali itapeleka fedha, kwa ajili ya kuhakikisha jengo hili linajengwa ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Name
Eng. Ezra John Chiwelesa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Biharamulo Magharibi
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 10
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, Vituo vya Afya vya Kalenge na Nyabusozi, vilitengewa pesa kiasi cha shilingi milioni 500. Je, ni lini pesa hii italetwa, kwa ajili ya ukarabati wa vituo hivyo?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Ezra Chiwelesa kwamba, Serikali ina nia thabiti ya kuhakikisha inaimarisha utoaji wa huduma za afya msingi na ndiyo maana inaleta fedha, kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika vituo hivi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, Serikali itaendelea kuleta fedha kwa awamu kama ilivyotanguliza kuleta fedha za awali kwa awamu iliyopita. Pia, awamu inayofuata fedha zitakuja, kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, vituo hivi vinaendelea kuboreshwa na vinajengwa ili wananchi waweze kupata huduma bora.
Name
Eng. Stella Martin Manyanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 11
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Hii nauliza mara ya tano, seriously. Kata ya Kihagara watu wanalala watano, wanne, kwenye kitanda. Ni lini wodi itajengwa katika Kijiji cha Kihagara, kwa ajili ya Kituo cha Afya Kihagara?
SPIKA: Mheshimiwa Stella Manyanya, kama unauliza mara ya tano ni swali la nyongeza, nafikiri lije la msingi ili ujibiwe swali lako kikamilifu, kwa sababu, kama ni mara ya tano, halafu unauliza kitu hicho hicho na bado majibu hayajakutosheleza, nashauri swali lako lije kama swali la msingi uweze kupata majibu mahususi, kwa ajili ya hicho kituo cha afya.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ni pamoja na maswali ya msingi.
SPIKA: Ulishauliza, hayo ni ya msingi?
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, nasema nilishauliza pia, swali la msingi kuhusiana na suala hili.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie pia, Mheshimiwa Engineer Manyanya kwamba, nia ya Serikali ni kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma za afya msingi. Ndiyo maana Serikali inatoa fedha kwa awamu, kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika vituo vyetu vya afya, hospitali na zahanati.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali kupitia Serikali Kuu na kupitia mapato ya halmashauri itaendelea kuleta fedha kwa awamu, kwa ajili ya kuendelea kuimarisha na kukamilisha miundombinu yote inayohitajika, ili wananchi waweze kupata huduma iliyo bora katika kituo hiki alichokitaja, Mheshimiwa Mbunge.
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha katika Kituo cha Afya Kisiwani – Same ili kukamilisha ujenzi wa majengo muhimu?
Supplementary Question 12
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niulize swali la nyongeza. Ni lini Serikali itajenga majengo ya watumishi na mortuary katika Kituo cha Afya cha Uru Kusini ili kiweze kuleta tija?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Felista Njau kwamba, Serikali inaendelea kuhakikisha inaimarisha huduma za afya msingi kwa kuendelea kujenga miundombinu imara, mizuri na kuikamilisha yote, ili wananchi waweze kupata huduma bora. Ninaomba nimhakikishie, Serikali itatenga fedha kila mwaka wa bajeti kupitia Serikali Kuu na kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, kwa ajili ya kuhakikisha inakuja kujenga na kukamilisha majengo aliyoyataja, Mheshimiwa Mbunge.