Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 2 2025-01-28

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:-

Je, kuna mkakati gani wa kupeleka huduma za jamii na kuboresha miundombinu ya shule zilizobaki katika Tarafa ya Ngorongoro?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kupeleka huduma za jamii na kuboresha miundombinu ya shule katika maeneo yote yenye uhitaji, ikiwemo Tarafa ya Ngorongoro ambapo mwaka 2021/2022 hadi mwaka 2023/2024 Serikali imetumia jumla ya shilingi bilioni 7.9 za ruzuku ya elimu bila malipo katika Tarafa ya Ngorongoro. Aidha, mwaka 2024/2025, Serikali imetoa shilingi bilioni 1.7 za ruzuku ya elimu bila malipo, kwa ajili ya kuboresha huduma za elimu katika Tarafa hiyo.

Mheshimiwa Spika, vilevile halmashauri kupitia mapato ya ndani, mwaka 2024/2025 imetoa jumla ya shilingi milioni 120, kwa ajili ya kukarabati miundombinu katika katika Shule za Msingi Alailelai, Sendui, Olchanimerock, Naiyobi, Nainokanoka, Olbalbal, Ngoile, Moklal na Oloilob.