Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kupeleka huduma za jamii na kuboresha miundombinu ya shule zilizobaki katika Tarafa ya Ngorongoro?

Supplementary Question 1

MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na jitihada hizi za Serikali, bado mazingira ya shule alizozitaja Mheshimiwa Naibu Waziri ni mabovu. Ninaomba, ikimpendeza, aweze kuzitembelea na kujionea mazingira halisi.

Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza; je, ni lini ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ngorongoro utafanyika na Serikali ikiwemo kuongeza mabweni?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Shule ya Sekondari ya Rift Valley, Wilayani Monduli, wana changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama. Je, ni lini Serikali itawachimbia kisima hawa wanafunzi wetu ili waweze kusoma vizuri?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nimepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na kufika, ili kujionea hali halisi katika Tarafa hii ya Ngorongoro, kwa maana ya Sekta hii ya Elimu. Pia, kuhusiana na swali la kwanza la Mheshimiwa Mbunge, ninaomba nimhakikishie kwamba, Serikali inaendelea kutenga fedha. Kama nilivyojibu kwenye majibu ya msingi kwamba, kupitia mapato ya ndani tayari kuna milioni 120 ambazo zimetengwa katika mwaka huu wa bajeti, ili kuhakikisha zinakarabati miundombinu katika shule.

Mheshimiwa Spika, Desemba, 2024, kupitia fedha shilingi milioni nane, matundu nane ya vyoo yamejengwa katika shule hiyo. Pia, tuna shilingi milioni 100 ambazo zipo, kwa ajili ya ujenzi wa bwalo. Kwa hiyo, nichukue nafasi hii kuendelea kumsisitiza mkurugenzi na timu yake ya elimu, waweze kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu hii, ili iweze kukamilika kwa wakati na wanafunzi wetu waweze kupata mazingira bora ya kusomea.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la pili la Mheshimiwa Zaytun Swai, kuhusiana na Shule hii ya Rift Valley ambayo haina kisima na haina maji; tayari Serikali imeshasambaza mitambo ya kuchimba visima, kila mkoa umepata mitambo hii, kwa ajili ya kuchimba visima. Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kumkumbusha mkurugenzi wajibu wa msingi, yeye pamoja na timu yake, waweze kufanya mawasiliano na Mamlaka ya Maji ya Mkoa, kupitia Ofisi ya RAS, ili waweze kuchimba kisima kwa gharama nafuu, ili wanafunzi wetu katika Shule hii ya Rift Valley waweze kupata maji na wawe na mazingira ya kusomea na walimu wawe na mazingira mazuri ya kufundishia.

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kupeleka huduma za jamii na kuboresha miundombinu ya shule zilizobaki katika Tarafa ya Ngorongoro?

Supplementary Question 2

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Je, ni lini miundombinu ya Shule ya Msingi Iyendwe, Siliwiti, Sanja, Mfuto pamoja na Ipatikana itaboreshwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia miradi mbalimbali, ukiwemo Mradi wa SEQUIP wa gharama ya jumla ya shilingi trilioni 1.2 na kupitia mapato ya ndani, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu katika Sekta ya Elimu. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tayari tumekuwa tukileta fedha kila awamu, kila mwaka wa bajeti, kwa ajili ya kuendeleza miundombinu katika Sekta ya Elimu. Nimhakikishie, Serikali itaendelea kufanya hivyo, ili kuzifikia shule hizi alizozitaja, ili ziweze kupatiwa miundombinu bora na wanafunzi wetu wapate sehemu nzuri ya kujifunzia na walimu wapate sehemu nzuri ya kufundishia.

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kupeleka huduma za jamii na kuboresha miundombinu ya shule zilizobaki katika Tarafa ya Ngorongoro?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Shule ya Sekondari SUA maboresho yake yatakamilika, hasa ujenzi wa maabara?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Chiristine Ishengoma kwamba, Serikali inaendelea kuleta fedha kwa awamu, kwa ajili ya kukamilisha miundombinu katika Sekta ya Elimu. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali italeta fedha, kwa ajili ya kukamilisha miundombinu hii ya maabara, ili wanafunzi waweze kupata miundombinu bora ya kupatia elimu.

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kupeleka huduma za jamii na kuboresha miundombinu ya shule zilizobaki katika Tarafa ya Ngorongoro?

Supplementary Question 4

MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itapeleka fedha kwenye shule kongwe zilizopo katika Jimbo la Newala Vijijini, ili ziweze kuboreshwa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kwamba, kuna shule ambazo ni kongwe, miundombinu yake imechakaa na inahitaji ukarabati au ujenzi wa shule mpya. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Maimuna Mtanda kwamba, Serikali kila mwaka wa fedha inafanya ukarabati katika shule zetu Kongwe.

Mheshimiwa Spika, nitakaa na Mheshimiwa Mbunge tutaongea kwa karibu, ili aweze kunieleza vipaumbele katika jimbo lake, ili katika mgao naye aweze kupata ujenzi na ukarabati wa shule hizi kongwe.

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kupeleka huduma za jamii na kuboresha miundombinu ya shule zilizobaki katika Tarafa ya Ngorongoro?

Supplementary Question 5

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, Shule ya Msingi Omuchwekano na Shule ya Msingi Kitwechenkura zimechakaa majengo, lakini pia, vyoo vikiwa vimekaribia kujaa. Ninataka kujua mkakati wa Serikali wa kuboresha majengo na pia, huduma ya vyoo ambavyo kwa sasa vinafurika na hakuna maji safi na salama?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nia na madhumuni ya Serikali ni kuhakikisha kwamba, inaboresha miundombinu katika Sekta ya Elimu kwa kuboresha ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama vile madarasa, kujenga mabweni, kukarabati vyoo na kadhalika. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, hili ni jukumu la msingi kabisa la Serikali na Serikali itaendelea na wajibu huo na kuja kuzifikia shule hizi ulizozitaja ambazo zina mazingira ambayo siyo mazuri kwa wanafunzi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, Serikali itafika kwenye shule hizo na itapeleka fedha kwa ajili ya kuhakikisha zinakarabatiwa.