Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 4 2025-01-28

Name

Abdulhafar Idrissa Juma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtoni

Primary Question

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA aliuliza:-

Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kushughulikia masuala ya usalama barabarani ikiwemo kuweka na kukarabati taa za barabarani zilizoharibika kote nchini. Kwa sasa, TANROADS ipo katika hatua ya manunuzi ya kuwapata wakandarasi watakaofanya kazi hiyo. Baada ya kukamilika kwa hatua ya manunuzi na wakandarasi kupatikana, kazi ya ukarabati na uwekaji wa taa hizo itafanyika kulingana na mahitaji ya kila Mkoa. Ahsante.