Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdulhafar Idrissa Juma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtoni

Primary Question

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine?

Supplementary Question 1

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA: Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha sasa tumeshazidi nusu. Je hiyo hatua ya manunuzi itaisha lini maana kiza kimezidi katika baadhi ya barabara?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimwa Spika, labda tu nimjulishe Mheshimiwa Mbunge kwamba kulikuwa na changamoto kubwa kwamba taa zilikuwa nyingi zinatofautiana na hazina standard. Kwa hiyo, tumeamua kununua kwa pamoja ili taa hizo ziwe katika ubora unaolingana katika nchi yote, ndiyo maana huo mchakato umechukua muda mrefu, lakini nimhakikishie kwamba tunavyoongea huu ni mwezi wa kwanza na tunaweka kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha huu tutakuwa tumerudisha taa zote ambazo zina uharibifu kwa namna yoyote ama zimegongwa ama zimeharibika. Ahsante.

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine?

Supplementary Question 2

MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimwa Spika, je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kufunga barabara katika Mji wa Mbinga? Ahsante.
SPIKA: Kufunga barabara ama kufunga taa?

MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimwa Spika, kufunga taa katika Mji wa Mbinga. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimwa Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi tumepata mahitaji ya Mikoa yote na Miji yote ambayo haina taa, ndiyo maana tunanunua taa kwa pamoja nikiamini kwamba Mji wa Mbinga nao utanufaika kupewa taa hizo kama Mji wa Mbinga una mahitaji ya hizo taa. Ahsante.

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itamalizia kufunga taa katika Mji wa Tinde hasa kutoka njia panda kwenda Kahama?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mahitaji ya taa yanaletwa na mkoa na Meneja wa Mkoa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumepata orodha ya mahitaji ya taa zote za barabarani, kwa hiyo ina uhakika na Mji wa Tinde utakuwa ni mji mmojawapo ambao utapata hizo na tutakuja kukamilisha kufunga hizo taa ambazo bado. Ahsante.

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine?

Supplementary Question 4

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimwa Spika, nini mpango wa Serikali kukarabati taa zilizoharibika za barabarani katika barabara za TANROADS Wilaya ya Kilwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hata katika jibu langu la msingi nimesema taa zote ambazo zimeharibika, zimegongwa ama hazifanyi kazi zimeshaainishwa na ndiyo maana tumenunua kwa pamoja ili ziende zikafungwe ikiwepo na Mji wa Mheshimiwa Mbunge wa Kilwa. Ahsante.

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine?

Supplementary Question 5

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimwa Spika, ahsante. Ni lini mkandarasi anaeweka taa katika Wilaya ya Nanyumbu atalipwa fedha zake ili kazi iendelee?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimwa Spika, ahsante. Ninaomba tu nilichukue hilo la Mheshimiwa Mbunge nijue changamoto ni nini. Kwa sababu tunachojibu hapa ni taa ambazo zimeharibika ama zimegongwa, kwa hiyo masuala ya malipo nitaomba baada ya hapa niweze kuongea na Mheshimiwa Mbunge ili nimpe jibu sahihi ni kitu gani kimekwamisha, ahsante.

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. ABDUL – HAFAR IDRISSA JUMA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa taa za barabarani zilizoharibika kwa kugongwa au hitilafu nyingine?

Supplementary Question 6

MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimwa Spika, Mji mdogo wa Iguguno una kipande cha kilomita moja tu ya lami, lakini hauna taa. Je, ni lini angalau mtatufariji tu kwa taa maana yake barabara yote hiyo ni ya vumbi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, tumesema mara kadhaa kwamba miji yote mikubwa na miji ambayo inakua itawekewa taa nina hakika hata Mji wa Iguguno ambao unakua utakuwa upo kwenye huo mpango na hasa kama Mheshimiwa Mbunge alifikisha ama Meneja wa Mkoa atakuwa ameleta maombi, kwa sababu tumekusanya maombi yote ya miji ambayo inakua ili iweze kuwekewa taa, ahsante.