Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 5 2025-01-28

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara kwa kutumia zege sehemu korofi ili kuepuka matengenezo ya mara kwa mara na upotevu wa fedha?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuboresha sehemu korofi katika barabara kama vile milima mikali, Mbuga na sehemu zenye udongo wa mfinyazi. Hatua hizo ni pamoja na ujenzi kwa kutumia zege, ujenzi kwa kutumia mawe na kadhalika. Pamoja na kuzingatia mahitaji, lakini pia uamuzi wa ujenzi wa aina gani utatumika kuzingatia gharama za upatikanaji wa mali ghafi za ujenzi zinazopatikana kwa urahisi katika eneo husika.