Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara kwa kutumia zege sehemu korofi ili kuepuka matengenezo ya mara kwa mara na upotevu wa fedha?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimwa Spika, namshukuru Waziri kwa majibu yake, upatikanaji wa malighafi kama alivyosema, sasa kwa kuwa vifaa vya kujenga barabara kwa zege hupatikana hapa Tanzania, tofauti na lami ambayo huagizwa kutoka nje. Sasa Serikali haioni iko haja kwamba zitaokolewa fedha nyingi na hivyo kuongeza barabara nyingi zaidi kujengwa badala ya kendelea na kutumia lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimwa Spika, ni kweli kwamba zipo malighafi ambazo zinapatikana Tanzania, lakini ninataka tu nimkumbushe Mheshimiwa Mbunge kwamba tunapoongelea zege si vifaa vyote vinapatikana hapa ndani. Vinavyopatikana ndani hapa ni mawe lakini cement pamoja na nondo ni vitu ambavyo lazima uvitumie kwenye ujenzi wa barabara ya zege na zege ina gharama kubwa zaidi kuliko aina ya lami, ndiyo maana tuna barabara chache sana tulizojenga kwa zege na gharama yake inaweza ikawa zaidi ya mara mbili na nusu kuliko barabara ya kawaida ya lami ukijenga kwa zege. Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri cement na nondo si zinapatikana hapa nchini? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimwa Spika, zinapatikana hapa lakini gharama yake unapojenga barabara maana yake ni kama unajenga msingi wa nyumba na ndiyo maana tuna barabara kwa mfano ile inayoenda Ludewa wakati huku unaweza ukajenga kilomita moja pengine bilioni moja na nusu kwa kilomita ile inakwenda si chini ya bilioni tatu kwa kilomita moja kwa sababu ya ujenzi wake unavyokuwa. Ahsante.

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara kwa kutumia zege sehemu korofi ili kuepuka matengenezo ya mara kwa mara na upotevu wa fedha?

Supplementary Question 2

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimwa Spika, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara kwa lami kutoka Mpomvu kwenda Kakora na kutoka Katoro kwenda Ushirombo? Ninashukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimwa Spika, ninaomba nimwombe Mheshimiwa Magessa Mbunge wa Busanda. Kwenye majibu yangu yalikuwa yanazungumzia maeneo korofi ambayo yanahitaji ujenzi wa zege. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge ili nimjibu vizuri kwa uhakika labda baada ya hapa niweze kujua hiyo barabara ambayo anaiongelea kwa ujenzi wa kipande cha lami, tuongee naye nijue tuko hatua gani kwa sababu tayari ipo kwenye mpango wa ujenzi nijue tuko kwenye hatua gani ili niweze kumpa jibu linaloeleweka. Ahsante.

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara kwa kutumia zege sehemu korofi ili kuepuka matengenezo ya mara kwa mara na upotevu wa fedha?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itafanya ukarabati mkubwa kwenye Barabara kuu ya Chalinze, Segera, Korogwe, Mombo, Same na Himo?

SPIKA: Maeneo korofi Mheshimiwa?

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, barabara hii inahitaji ukarabati mkubwa maeneo mengi ni korofi.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwanza hiyo barabara aliyoitaja ni barabara ya zamani ambayo pia ni barabara ambayo ni nyembamba sana. Sasa hivi tumeshafanya usanifu wa barabara yote ambayo itakuwa ni kuifanyia ukarabati mkubwa kama kuijenga upya kwa sababu ya hali yake na vile ambavyo ni nyembamba inatakiwa ukarabati mkubwa wala siyo kujenga eneo korofi ni kama barabara yote inatakiwa ikarabatiwe. Ahsante.