Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 21 2025-01-29

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:-

Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Vituo vya Afya Kata za Misughaa, Issuna na Mang’onyi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uwepo wa kata ambazo hazina vituo vya afya kote nchini ikiwemo Kata za Issuna, Misughaa na Mang’onyi katika Jimbo la Singida Mashariki. Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilipeleka shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya vya Ntuntu na Iglanson katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Ikungi itatenga shilingi milioni 100 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Issuna. Kata za Misughaa na Mang’onyi zitajengewa vituo vya afya kwa awamu kwa kuzingatia mahitaji na vigezo vilivyoainishwa.