Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Miraji Jumanne Mtaturu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mashariki
Primary Question
MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Vituo vya Afya Kata za Misughaa, Issuna na Mang’onyi?
Supplementary Question 1
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Nichukue nafasi hii kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; ni kwamba Jimbo la Singida Mashariki lina kata 13, lakini vituo vya afya vipo kwenye kata mbili tu ambazo ni Ntuntu pamoja na Unyahati, kata 11 hazina vituo. Ninaomba nipate majibu ya Serikali kwamba, kata za kimkakati nilipeleka Misughaa ambayo tulitarajia kupelekewa fedha mpaka leo hatujapata, lakini Kata ya Issuna, Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Emmanuel Nchimbi alishasema kituo hicho kijengwe mapema kabla ya uchaguzi. Sasa ninaomba nipate jibu la Serikali, ni lini sasa fedha hizo zitapelekwa kwa ajili ya kujenga vituo hivyo? Ahsante sana.
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Kituo hiki cha Afya cha Ntuntu ni miaka mitatu kama alivyosema kimepelekewa fedha, hakijakamilika mpaka sasa kwa kutoa huduma, ni OPD pekee yake inafanya kazi, jengo la mama na mtoto ambalo ilikuwa ni lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto havijakamilika. Ninaomba kujua commitment ya Serikali, imeshanijibu hapa itapeleka baada ya miaka miezi miwili, miezi miwili imeshapita. Ninaomba kujua ni lini sasa ...
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, ni lini sasa kituo hicho kitajengwa ili wananchi wale waweze kupata huduma hiyo ya afya? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, kwanza ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri ya uwakilishi anayoifanya katika jimbo lake.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na maswali yake mawili; kuhusiana na swali la kwanza, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuhakikisha inaimarisha huduma za afya msingi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali katika huu mwaka wa fedha italeta fedha shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza kujenga kituo cha afya cha mkakati katika majimbo yote ya Tanzania Bara, ikiwemo katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge la Singida Mashariki.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ahadi za viongozi ni kipaumbele namba moja katika mipango na utekelezaji wa shughuli za Serikali. Nimhakikishie kwamba ahadi ya kujenga kituo cha afya katika Kata ya Issuna kitatekelezwa na Serikali inatafuta fedha ili ihakikishe ahadi iliyotolewa na kiongozi wetu, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la pili la Mheshimiwa Mbunge, ninaomba nichukue nafasi hii kumkumbusha Mkurugenzi wa Halmashauri aweze kutumiza wajibu wake wa msingi, kwa sababu fedha zilishaletwa kwa ajili ya kuhakikisha Kituo hiki cha Afya cha Ntuntu kinajengwa, asimamie na kama kuna fedha zimepungua aongeze kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ili majengo haya muhimu hasa ya mama na mtoto yaweze kukamilika na huduma ya afya iweze kutolewa kwa wananchi. (Makofi)
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Vituo vya Afya Kata za Misughaa, Issuna na Mang’onyi?
Supplementary Question 2
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, ni kama alishajibu, nilitaka kuuliza je, ni lini Serikali itajenga kituo cha kimkakati katika Kata ya Old Moshi Mashariki? Ninakushukuru.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Profesa Ndakidemi kwamba Serikali katika huu mwaka wa fedha italeta fedha shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati katika majimbo yote Tanzania Bara ikiwemo Kituo hiki cha Afya alichokitaja cha Old Moshi Mashariki.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved