Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 53 2025-01-31

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaongeza Posho kwa Madiwani kwa kuwa wanafanya kazi kubwa kwenye Kata zao?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Waheshimiwa Madiwani katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, kutokana na Halmashauri kuwa na uwezo mdogo wa mapato ya ndani ya kulipa posho za Waheshimiwa Madiwani, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022, ilianza kulipa posho kwa Waheshimiwa Madiwani katika Halmashauri 168 kati ya 184 zilizopo. Katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2023/2024 jumla ya shilingi bilioni 63.9 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa posho za Madiwani.

Mheshimiwa Spika, posho za Waheshimiwa Madiwani bado hazikidhi mahitaji kutokana na Halmashauri nyingi kutokuwa na uwezo wa kulipa kupitia mapato ya ndani. Aidha, Serikali imeendelea kubuni vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri ili hatimaye posho za Waheshimiwa Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa zilipwe kwa ufanisi zaidi.