Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza Posho kwa Madiwani kwa kuwa wanafanya kazi kubwa kwenye Kata zao?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kusema kweli Madiwani wetu hawa wanafanya kazi kubwa sana katika nchi yetu, nasi Waheshimiwa Wabunge tumekuwa mbele mno kuwatetea Madiwani kupata haki zao zile za posho.
Mheshimiwa Spika, kwa sababu halmashauri nyingi zina mapato na halmashauri nyingine hazina mapato, naiomba Serikali ifanye uchambuzi wa kutosha kwa zile halmashauri ambazo hazina mapato ya kutosha kwa mwaka huu wa fedha 2025, wawaongezee kipato Madiwani wale kutoka shilingi 350,000 kuwa hata shilingi 500,000, kwa sababu Madiwani wao wenyewe, ukiongeza ni 150,000 tu. Naiomba Serikali kwa bajeti hii iweze kuleta bajeti ya Madiwani kwa halmashauri zile ambazo hazina uwezo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa tuna Sheria Na. 8 na Na. 7, utaratibu ule wa Mwongozo kwa Serikali za Vijiji, Jimbo la Bunda, vijiji na vitongoji vyake vingi havipati mapato yao. Naomba kwenye maeneo ambayo kuna mapato ya Serikali kwenye minada, masoko na kwenye mitera, ile sheria ya kurudisha 20% kwenye vijiji irudishwe kwenye mpango wake wa kila siku ambao ulikuwa unapangwa na Serikali kwa sababu sasa hivi hairudishwi kabisa, lakini kuna maeneo ya minada na masoko ambayo yanatoa ushuru kwenye maeneo hayo. Naiomba Serikali ifikirie jambo hilo kwa upana zaidi. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba nipokee maombi mazuri sana ya Mheshimiwa Getere, nasi kama Serikali tutayachakata na kuweka kwenye mipango kwa ajili ya utekelezaji.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved