Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 54 2025-01-31

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: -

Je, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha maeneo ya majiji na miji yanakuwa safi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maeneo ya miji na majiji yanakuwa safi, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutenga bajeti ya kuboresha miundombinu ya uondoshaji taka, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2023/2024 jumla ya shilingi bilioni 22.3 zilitengwa na shilingi bilioni 22.1 zilitumika. Aidha, shilingi bilioni 10.3 zimetengwa katika bajeti ya 2024/2025 kwa ajili ya shughuli za usafi wa mazingira katika majiji.

Mheshimiwa Spika, mikakati mingine ni pamoja na ushirikishwaji wa mamlaka mbalimbali za umma zenye wajibu kisheria wa kusimamia usafi ikiwemo TARURA na TANROAD, matumizi ya kampuni binafsi za usafi, uhamasishaji na utoaji wa elimu ya usafi wa mazingira kwa jamii, ushirikishwaji wa wadau katika kuanzisha vituo vya uchakataji na urejelezaji wa taka pamoja na utekelezaji wa sheria ndogo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa pamoja na jitihada hizi, bado usafi wa baadhi ya miji hauridhishi. Hivyo, itaendelea kuhakikisha usafi unafanyika kikamilifu ili majiji na miji iwe kivutio kwa jamii na wageni pamoja na kuzuia magonjwa yatokanayo na uchafu.