Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 55 2025-01-31

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Sanga Mwalugesha, Wilaya ya Maswa?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 na 2023/2024 Serikali ilipeleka shilingi bilioni 1.9 katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa ajili ya ukarabari wa hospitali pamoja na ujenzi wa Vituo viwili vya Shishiyu na Badi. Aidha, ujenzi na ukarabati wa hospitali ya wilaya pamoja na vituo vya afya umekamilika na vinatoa huduma.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati zilizokidhi vigezo ikiwemo Kata ya Sanga Mwalugesha.